Mawaziri nchini Zambia wamemtaka Rais anayeshikilia madaraka ya nchi hiyo Guy Scott kuachia ngazi kwa madai hawana imani nae, yani kiongozi mweupe kushikilia madaraka kitu ambacho hakijawahi kutokea zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Scott alipewa madaraka baada ya rais wa nchi hiyo Michael Satta kufariki October 2014 ambapo baada ya hiyo, sasa mawaziri 14 kati ya 17 waliohudhuria mkutano ulioitishwa na kupiga kura ya kutaka Rais huyo aachie madaraka kwa kukosa imani naye kutokana na asili yake, wamepiga kura ya ndio.
Scott amekua katika wakati mgumu kutokana na kutokua raia wa nchi hiyo lakini hata hivyo imebakia mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
RSS Feed
Twitter
09:25
NGOSHA TV
0 comments:
Post a Comment