Friday, 2 January 2015



Ndugu zangu....
Mpira wa miguu unaongoza duniani kuwa na mashabiki wengi zaidi.Hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika mchezo huo.
Hakika kwa sasa soka ni biashara nzuri zaidi duniani.Una shangaa nini tazama matajiri wanavyopigana vikumbo kuwania umiliki wa vilabu mbali mbali barani ulaya.
Uku wana soka kutoka Afrika magharibi wakichuana vikali kuchukua noti kutoka ulaya.Wana soka wetu wa hapa nyumbani wao wana kwenda hatua mbili wana rudi nane na kujipongeza.
Una kumbuka wakati Haruna Moshi Boban hakiwa kwenye ubora wake..?
Yeye alipata nafasi ya kusukuma kandanda barani ulaya kwenye nchi ya Sweden.Lakini kwa sasa unajua yuko wapi....Boban yuko na timu ya Friends Rangers inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Huu ni sawa na utani katika soka letu,ambalo limekosa mipango thabiti kutoka kwa viongozi wetu wa soka.
Lakini si hilo tu eti hata mshahara wake pale Friends Rangers analipwa na msanii wa mziki wa kizazi kipya... Diamond kiasi cha shilingi za Kitanzania 400000.Huu pia ni utani unaokera zaidi.


Mwanamfalme Andrew
Kasri ya Buckingham imepinga madai kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa alijihusisha katika tabia mbaya baada ya kubainika kwa nakala za mahakamani nchini Marekani zinazomuhusisha na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
Taarifa ya kasri hiyo imeelezea madai hayo kwamba mwanamfalme huyo alifanya tendo la ngono na msichana mdogo kama yasio kuwa ya kweli.
Mamaake mwanamfalme Andrew
Tuhuma hizo zimetolewa katika kesi inayomuhusisha rafiki moja wa zamani wa mwanamfalme Andrew, tajiri Jefferey Epstein ambaye ameshtakiwa kwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia.
Katika nakala zilizopatikana katika mahakama ya huko Florida,mwanamke mmoja anadai kwamba alilazimishwa na Epstein kufanya tendo la ngono na watu wengine akiwemo mwanamfalme huyo wakati msichana huyo alipokuwa na miaka 17,ambao ni umri mdogo wa kuweza kuruhusu tendo kama hilo nchini Marekani.


o
Rais wa Gambia yahya Jammeh aliyeepuka jaribio la mapinduzi.baadhi ya watu waliohusika na mapinduzi hao wameanza kukamatwa
Watu kadhaa wamekamatwa na kuzuiliwa, kufuatia jaribio la mapinduzi ya hapo Jumanne dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo, Yahya Jammeh.
Waliokamatwa ni pamoja na maafisa kadhaa wa kijeshi pamoja na raia.
Wanajeshi watiifu kwa rais, wanasemekana wamekuwa wakisaka nyumba za wapinzani wake.
Awali akiwa katika mji mkuu Banjul, Rais Jammeh alilaani washukiwa hao wa mapinduzi wanaosemekana kuungwa mkono na baadhi ya mataifa ya kigeni.


Mmoja ya watoto waliojeruhiwa wakati bomu liliporushwa katika nyumba moja iliokuwa ikifanya sherehe ya harusi mkoani Helmand nchini Afghanistan.Takriban watu 20 waliaga dunia
Sherehe moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya kumi na mbili.
Kisa hicho kilitokea wakati wa makabiliano makali kati ya walinda usalama wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Helmand.
Mmiliki wa jumba lilofanyiwa harusi hiyo amesema kuwa wageni walikuwa wanajikusanya nje kumkaribisha bi harusi,na kuongezea kuwa watoto wake tisa wametoweka.
Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Lashkar Gah,mji mkuu wa mkoa huo.
Shambulio hilo limetokea wakati wa siku ya mwisho kwa ujumbe wa wanajeshi wa Marekani na wale wa shirika la kujihami la NATO wanaoondoka nchini Afghanistan.


Wastara Asoma Dua Kumuenzi Sajuki
  • Wastara Asoma Dua Kumuenzi Sajuki 1
 
Mwigizaji wa filamu za Kibongo Wastara Juma leo amesoma dua  maalumu kama ishara ya kumkumbuka na kumuenzi aliyekuwa mume wake kipenzi , marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Marehemu Sajuki alifariki dunia Januari 2.2013 , ambapo leo ametimiza miaka  miwili, dua ya kumuombea ilianzia katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo marehemu Sajuki alizikwa na baadae kuhamia nyumbani kwake Tabata.
Akizungumza na GPL, Wastara alisema anajisikia faraja sana kusoma dua kwa ajili ya mtu aliyempenda lakini pia anawashukuru wadau na  wote waliojitokeza katika kufanikisha  kisomo hicho.
Aidha wasanii mbalimbali wamejitokeza akiwemo Mohamed Mwikonge ‘’Frank’ Mtitu, Nisha, Bond na wengineo ambao pia wameomba na kuwakumbusha wasanii na wadau mbalimbali kuwakumbuka na kuwaenzi wasanii pindi wanapoaga dunia.


mahakama ya kenya
Mahakama kuu nchini Kenya imesimamisha kwa muda matumizi ya baadhi ya vipengee vya sheria ya usalama yenye utata iliopitishwa na bunge na kuidhinishwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Wanasiasa wa upinzani waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uhalali wa sheria hiyo kikatiba, huku wakisema inahujumu haki ya raia wa Kenya.
Sheria hiyo iliidhinishwa majuma mawili yaliyopita bungeni huku wabunge wa upinzani na serikali wakikabiliana kwa makonde na mateke.
Bunge la Kenya
Serikali ya Kenya inasema kuwa sheria hiyo itasaidia kukabiliana na makundi ya igaidi kama vile lile la Al-Shabab.
Lakini upinzani umeibua utata kuhusu baadhi ya vipengee, kama kile cha kuwazuilia washukiwa hadi mwaka mmoja bila ya kufunguliwa mashtaka wakisema kinahujumu uhuru wa raia.
Design by Victor Simon -