
Ndugu zangu....
Mpira wa miguu unaongoza duniani kuwa na mashabiki wengi zaidi.Hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika mchezo huo.
Hakika kwa sasa soka ni biashara nzuri zaidi duniani.Una shangaa nini tazama matajiri wanavyopigana vikumbo kuwania umiliki wa vilabu mbali mbali barani ulaya.
Uku wana soka kutoka Afrika magharibi wakichuana vikali kuchukua noti kutoka ulaya.Wana soka wetu wa hapa nyumbani wao wana kwenda hatua mbili wana rudi nane na kujipongeza.
Una kumbuka wakati Haruna Moshi Boban hakiwa kwenye ubora wake..?
Yeye alipata nafasi ya kusukuma kandanda barani ulaya kwenye nchi ya Sweden.Lakini kwa sasa unajua yuko wapi....Boban yuko na timu ya Friends Rangers inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Huu ni sawa na utani katika soka letu,ambalo limekosa mipango thabiti kutoka kwa viongozi wetu wa soka.
Lakini si hilo tu eti hata mshahara wake pale Friends Rangers analipwa na msanii wa mziki wa kizazi kipya... Diamond kiasi cha shilingi za Kitanzania 400000.Huu pia ni utani unaokera zaidi.
0 comments:
Post a Comment