
Ndugu zangu bado naendelea na Town Tour hapa Singida Mkoa ambao ninajivunia kuzaliwa hapa kwani hapo baadaye nitautangaza kadri ya uwezo.
Nilipofika kwa bibi nimekaribishwa na kinywaji cha asili kinaitwa togwa ama magai lakini kinywaji hicho kipo kwenye kipeyu aina ya chombo ambacho kinatengenezwa kutokana na kibuyu kwa wakazi wa Singida watakuwa wananielewa vizuri.
Naam narejea kwenye somo la asili na asilia ya mtanzania wa Singida ni Magai/Togwa yakiwa kwenye kipeyu sio Soda ikiwa kwenye glass ama chupa
0 comments:
Post a Comment