Friday, 19 December 2014


Nisha: Wezi Wa Kazi Zetu Wanatushusha....Shabiki Nini Kifanyike?
  • Nisha: Wezi Wa Kazi Zetu Wanatushusha....Shabiki Nini Kifanyike? 1
 
Ikiwa ni  siku tatu tu! zimebaki kutoa  movie yake mpya HAKUNA MATATA mwigizaji wa kike wa filam hapa bongo, Salma Jabu Nisha kupitia mtandaoni ameonyesha kuumizwa naswala zima la wezi wa kazi za wasanii hapa nchini na kusema ndio kitu pekee kinachaowarudisha nyuma, katika kuelezea swala hilo akaomba mchango wa mawazo ya jinsi ya kulitatua taizo hili.
Nanukuu;
"Swala la msanii kuibiwa ni swala sugu sana,wewe shabiki yetu tukipotea kwenye tasnia utajiskiaje?
Kikubwa kazi zetu zinaibiwa sana na hatupati faida wezi ndo wanaonufaika, Kuanzia machinga anayeuza cd fake,library anayekodisha cd 1 mara 100 na kuendelea, Linauma sana hili swala mashabiki zetu,waandishi wa habari,blog zote tunaomba msaada katika kupiga vita Hali hii.. Epuka cd fake,nunua original kumkomboa msanii wako na Taifa kwa ujumla".
Aliendelea;
"Au niwaulize nini kifanyike? Na kwa upande wako unaona wizi wa kazi za wasanii nani chanzo? Serikali inatulipisha kodi kila siku lakini kutetea haki yetu kuibiwa hamna msaada,si kwa bongo flavor wala bongo movie. Tujiulize kwanini wasanii wa music hawauzi albam sa hivi? au kwanini soko la filamu linashuka ukweli ni kwamba wezi wanatushusha tunapiga vita sana ila ila bado tatizo linaongezeka".
Sisi kama Bongomovies.com kwa nguvu zote tunapinga na kukemea vitendo vyote vinavyopelekea wasanii kupoteza mapato ya kazi zao. Lakini tunaamini wewe shabiki ndio unaweza kupunguza tatito hili kwa kununua kazi zao “original”. TUWAUNGE MKONO WASANII WETU.


0 comments:

Post a Comment

Design by Victor Simon -