Wageni na maafisa wa shirika la ndege la Etihad
wakishiriki katika hafla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shirika
hilo hapa nchini.
(Washiriki)
-
Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi Wa Umoja wa
falme za Kiarabu nchini Tanzania (Katikati)
-
Daniel Barranger, Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa
wa shirika la ndege la Etihad (wa nne kulia)
-
Dr. Shaaban Mwinjaka Katibu Mkuu, Wizara Ya Uchukuzi
(wa pili kulia)
-
Mh. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Kwa
Umoja wa falme za Kiarabu (wa nne kushoto)
-
Mhandisi Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege-Tanzania
(wa kwanza kushoto)
-
Ahmed
Al Shehhi-Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ndege la Etihad Tanzania (wa kwanza kulia
Ndege iliyozinduliwa na Shirika la Ndege la
Etihad ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam na kupokelewa na magari ya zimamoto kwa kumwaga maji kuashiria uzinduzi
rasmi wa Safari za ndege za shirika la ndege la Etihad lenye makao mkuu
Abudhabi. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja
kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika
la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger (katikati) akifurahia kikundi cha ngoma
mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika hilo la ndege hapa nchini. Uzinduzi huo
ulifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
ambapo sasa wateja mbalimbali watakua na fursa ya kusafiri moja kwa moja kutoka
Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.(VICTOR)
Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika
la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger akisalimiana na Balozi wa Umoja wa
falme za Kiarabu nchini Tanzania Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi mara baada ya
uzinduzi rasmi wa shirika hilo uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Julius Nyerere jijiji Dar es salaam. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa
watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka
Dar es salaam mpaka Abudhabi.
Makamu wa Rais- Mauzo Kimataifa wa shirika la
ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger (kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa shirika la ndege la Etihad
ambao ulifanyika siku ya jana jijini Dar es salaam.Pamoja nae ni Mh. Balozi wa
Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi,
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika la ndege la Etihad hapa
nchini. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja
kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.
Shirika la ndege la
Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za Kiarabu, leo hii imeendelea kuimarisha
uwepo wake Afrika Mashariki kwa kuzindua huduma zake mpya za safari za ndege
baina ya Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi nchini Tanzania na Abu Dhabi, mji mkuu
wa Falme za kiarabu (UAE).
Mara baada ya ndege
inayozinduliwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, ililakiwa
na mizinga ya maji kama ishara ya heshima kubwa na abiria walioshuka
wakikaribishwa kwa burudani ya ngoma za kitamaduni za Tanzania.
Shughuli ya kukata
utepe ilifuatia ambayo katika kuweka kumbukumbu ya tukio hilo la kufana ambapo
lilifanikishwa na
-
Dr
Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi
-
Dr
Adelhelm James Meru, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Maliasili
-
H.E.
Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Nchi za Falme za kiarabu
-
H.E.
Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi wa Nchi za Falme za kiarabu Tanzania
-
Daniel
Barranger, Makamu wa Rais wa Mauzo ya kimataifa wa shirika
la ndege la Etihad
-
Mhandisi:Thomas Haule Mkurugenzi
Mamlaka ya Ndege
Dar es Salaam imekuwa ni
kituo cha tatu kwa shirika la ndege la Etihad Afrika Mashariki, baada ya
Nairobi na Entebbe,na ya tisa barani Afrika.
Huduma hii mpya ikiwa
inaendeshwa na ndege aina ya Airbus A320 yenye madaraja mawili, siti 16 daraja
la “Business” na siti 120 daraja la “Economy” ikiwa imelenga wafanya biashara
na wanaosafiri kwa starehe moja kwa moja kila siku baina ya Dar es salaam na
Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji mrahisi kwenda nchi nyingine ukanda wa GCC,
Ulaya, India, Asia kaskazini, Asia ya Kusini na Australia.
Bw. Barranger,
alisema “uzinduzi huu wa safari za shirika la ndege la Etihad kuja Dar es
Salaam zimewiana na mkakati wetu wa kulenga masoko yanayo endelea kukua kwa
kasi”.
“Dar es Salaam ni mji
ambao umekuwa kivutio sana kwa watalii wanaotaka kufahamu tamaduni na historia
ya Tanzania, pia ni mlango wa vivutio vya kitalii vingi vya kitaifa na
kimataifa ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama kama Serengeti na kisiwa
cha Zanzibar.
“Nchi Falme za kiarabu
ni mdau mkubwa wa kibiashara na Tanzania, huduma hii mpya itaongeza nguvu
ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili. Ratiba za safari za ndege
zitawapa wageni urahisi wa kupata ndege za kuunganisha safari kwenda nchi
nyingine, ikiwa inahudumia safari nyingi sana baina ya Tanzania na nchi nyingi
katika mtandao wetu wa kimataifa kama Ahmedabad na Mumbai nchini India au
Beijing na Shanghai nchini China.”
“Pamoja na kutoa
huduma ya moja kwa moja kwa watalii na wafanya biashara baina ya nchi hizi
mbili, safari hizi pia zimeendelea kuimarisha uwepo wetu Afrika Mashariki na
Afrika kwa ujumla” aliongezea.
Shirika la ndege la
Etihad limekuwa likiongeza uwepo wake barani Afrika tokea walipozindua safari
zake za kwanza barani Afrika, huko Cairo November 2004. Baada ya hapo
zikafuatia Casablanca, Entebbe, Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, (15
January 2015) na Mahe huko visiwa vya shelisheli na mipango ya uzinduzi katika
mji wa Rabat, Morocco katikati ya mwezi Januari 2016.
Flight No.
|
Kutoka
|
Kuondoka
|
Kwenda
|
Kufika
|
Idadi
|
Ndege
|
EY681
|
Abu
Dhabi (AUH)
|
8:20
|
Dar es Salaam (DAR)
|
13:00
|
Kila Siku
|
A320
|
EY682
|
Dar es Salaam (DAR)
|
13:50
|
Abu
Dhabi (AUH)
|
20:15
|
Kila Siku
|
A320
|
Ratiba
za shirika la ndege la Etihad, Dar es Salaam kuanzia tarehe 1 December 2015:
Zingatia: Muda wa
kuondoka ni majira ya Dar es Salaam.
-
Mwisho-
Kuhusu
Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la
Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003na hadi kufikia mwaka 2014,
ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko
Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri
na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia,
Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing
takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66,
Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
0 comments:
Post a Comment