Kauli hiyo ya Mwakyembe inakuja kufuatia siku za hivi karibuni kutokea mvutano mkubwa kati ya wawili hao.
Mwakyembe amesema haamini kama tatizo ni kubwa kiivyo bali ni kitu chenye afya tu kwa sababu kinaleta ushindani mzuri ambao unapeleka muziki katika ngazi nyingine.
Mwakyembe amesema kuwa “Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate miziki mizito,”.
SIKU CHECHE ZILIZO PITA RAFIKI YANGU NA MWANAHABARI MWENZANGU Kione Hamis Mahuruku ALIANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK KUHUSU BIFU HILO.
MTAZAMO WAKE KWA KIASI KIKUBWA HUKO SAWA NA WA WAZIRI MWAKYEMBE.
........Hapa chini nimekuwekea andiko la Kione Hamis Mahuruku...soma kwa afya ya ubongo wako.
WAKIPATANA WATAJIMALIZA
Gaboooon.........! Itikia,mpaka Kombe la Dunia.......!
Hiyo ilikuwa Kauli Mbiu ya kuipa nguvu Timu yetu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17.Kuelekea Fainali na pengine tungefanikiwa kupita hatua ya Nusu Fainali tungeenda India katika Fainali za Dunia za Umri huo.
Nasib Abdull(Diamond Platnumz) na Alli Kiba(King Kiba),walihusishwa katika kampeni zile ile wafanye wimbo wa pamoja kwa ajili ya Hamasa kwa Watanzania.Wazo na msukumo ulitoka kwa Mheshimiwa Nape Moses Nnauye(MB) wa jimbo la Mtama mkoani Lindi wakati huo akiwa Waziri mwenye Dhamana ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Wazo la kuwakutanisha Wasanii hao halikuwa wazo baya,lakini lingeweza kuporomosha Biashara yao ya Muziki kama inavyokiki sasa.
Inahitaji Jicho la mbali kutambua kwa nini hawa jamaa walikwepana katika'kutia vocal' kwenye mdundo tulioaminishwa ulishanyongwa.
WASIOJUA
Mwanzoni mwa miaka ya 2000,kuliwahi tokea Ugomvi wa Wafalme wa TEMEKE(TMK),si wengine hao ni Juma Kassimu'Juma Nature-Kibla' dhidi ya Haroun Kahena'Inspector Haroun-Babu'.
Ilikuwa zaidi ya 'Bifu',ilikuwa zaidi ya 'Beto'.Nini hizi kelele za Mashabiki wa Mitandaoni! Kipindi kile hakuna Mitandao ya kijamii na hata Simu zilikuwa chache.Na kumiliki Simu ilikuwa big inshu.Kama unabisha tafuta Video ya ZEZE ft TID ft Jay Moe ujionee walivyozipa thamani Simu.
Wafalme hawa wa TMK,walikuwa na nguvu kila Kona ya nchi hii,na ndio maana ilikuwa Vita kubwa sana ya Watoto wa Uswahilini wenyewe wa wenyewe.
KUMBUKA
Inspector Haroun na Juma Nature pia kabla ya Vita yao nao wana historia inayoshabihiana na hawa Nguli wa sasa yaani Diamond na Kiba.Yaani kabla Vita yao walikuwa'Washikaji kinyama'.
Inspector Haroun alianza kutoka katika Game,na baadae Juma Nature akafuatia na kumpoteza Babu.Ndipo Wachochezi wakafanya yao,Ugomvi mkubwa ukatokea.
Ni kama hivi leo tu,Kiba alianza kutoka.Baadae Diamond akafuatia na akampoteza Kiba.Tofauti leo kuna Timu ambazo si za mpira.Kuna 'Team Diamond na Team Kiba'.
Hakuna mwenye akili timamu anayependa kuchochea Ugomvi tu kama yupo ana matatizo.Wanachokifanya hawa 'Mabwana wadogo' ni jambo zuri sana.Wao kama wao wanashindana katika Muziki.Tatizo hizo Timu zao ndio zinashambuliana sana.
KUMBUKA NA HII
Mfalme wa Rhymes Selemani Msindi'Afande Sele' na mdogo wake wa Mji kasoro Bahari mwenzake Philipo Nyandindi'O-Ten'.Hawa walikuwa na Bifu kubwa,ilisumbua sana.Katika Bifu hii ilimnufaisha sana O-Ten,kwani hakuwa na Ngoma za maana zaidi ya wimbo wake wa'Nicheki',tofauti na Afande yeye alishafahamika Bongo nzima.
NA HII
Godfrey Tumaini(Dudu Baya) Vs Lucas Mkenda(Mr.Nice).
Hawa haikuwa Bifu ya Kimuziki,waweza kuita ni ujinga,maana wao waliamua kupigana na siyo kushindana Kimuziki.
KWA NINI NASEMA DIAMOND NA KIBA WAKIPATANISHWA WATAJIMALIZA?
Tumeona Hatma za hao watangulizi wao katika Muziki.Watu walilalamika sana......'ooh....hakuna Muziki vijana wanakoelekea kubaya'
Ni kweli kulikuwa kubaya,hata ungekuwa wewe ndio mzazi wa Mr.Nice,ungejisikia vizuri mwano kupigwa na Dudu Baya?
Tanzania tunaamini katika Amani pamoja na Utu,wenye Busara wakaanzia mbaaaali.Babu na Kibla wakapatanishwa,Afande Sele na O-Ten yakamalizwa.Na hata waliopigana Dudu Baya na Mr.Nice wakipatanishwa.
NINI KILICHOFUATA?
Kilichofuata,hakuna tena ushindani wa Kimuziki,hata Kambi za EAST COAST TEAM na WANAUME TMK wakawa marafiki wakati awali walikuwa Mahasimu wakubwa.Wengi wao waliogopa kupeana changamoto za kimuziki walijua wakisemana kidogo tu katika Muziki wangesemwa wanachochea Bifu.
Muziki ukakosa ushindani,muziki ukakosa Changamoto.Ikafika wakati hata Taarabu ikarudi kwa kishindo wakati Afande Sele alishaiimba imepotea.
Kila kona watu wakawa wanamsikiliza Hadija Shaib'Dida' ama Geah Habib.Ndio,Taarab ilishika haswa.
Siku zikapita,mara DIAMOND vs KIBA,kelele zinapigwa kwamba wana Bifu.Mara zote wenyewe wanakanusha hawana Bifu.Sasa mimi nani hadi niseme wana Bifu?
#MsipataneFanyeniBiashara.
0 comments:
Post a Comment