Kamanda wa UVCCM Wilaya Iringa mjini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, Frederick Mwakalebela (kushoto) amekabidhi vifaa vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni nane (8m/-) kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa mjini Abedi Kiponza (wa pili kushoto) na Katibu wa CCM Zongo Lobo Zongo (wa pili kulia) kwa ajili ya kusaidia shughuli za chama katika masuala ya kunadi sera na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010. Shughuli hiyo ilikwenda sambamba na kumuaga aliyekuwa mkuu wa mkoa wa iringa Dkt. Christine Ishengoma kichama ngazi ya wilaya.
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways linasema limepata hasara ya dola milioni 116 katika kipindi cha nusu mwaka kinachomalizika mwezi huu wa Novemba.
Shirika hilo linasema hasara hiyo imetokana na mlipuko wa Ebola katika nchi tatu za Afrika Magharibi na kuzorota kwa hali ya usalama.
Mwandishi wa BBC aliyefuatilia taarifa hiyo Emmanuel Igunza anasema kuwa huu ni mwaka wa pili kwa kampuni hiyo kurekodi hasara. Idadi ya wasafiri imepungua mwaka huu kutokana na taarifa kuhusu hali mbaya ya usalama nchini Kenya.