BAADA ya kuachwa katika uteuzi wa wakuu wa mikoa ,alisekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma (pichani)amewaaga wakazi wa mkoa wa Iringa kwa kuchangia kiasi cha Tsh milioni 19 kwa ajili ya kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.
Dr Ishengoma akifungua moja kati ya vikao vya RCC Iringa kulia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba
Akizungumza katika mahojiano maalum na mtandao wa www.matukiodaima.co.tz leo , Dr Ishengoma ambae ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Morogoro (CCM) alisema kuwa pamoja na kutemwa katika nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa ila bado anampongeza sana Rais Profesa Jakaya Kikwete kwa uteuzi wake kama mkuu wa mkoa nafasi iliyoishi mapema mwezi huu baada ya rais kuteua wakuu wa mikoa wapya wanne na kufanya mabadiliko kwa maadhi ya wakuu wa mikoa nchini na Iringa nafasi yake kuteuliwa Bi Amina Juma Masenza .
Dr Ishengoma alisema kuwa kabla ya uteuzi huo alikuwa akiendelea na utekelezaji wa majukumu yake mbali mbali ya kupigania maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuwa siku moja kabla ya uteuzi huo alianza zoezi la kuhamasisa ujenzi wa maabara kwa kuanza kukabidhi mabati 150 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zoezi ambalo alikusudia kulifanya katika Halmashauri zote na fedha hizo za kununua mabati kiasi cha Tsh milioni 19 amelazimika kuzikabidhi kwa katibu tawala wa mkoa wa Iringa ili kuzikabidhi katika Halmashauri zilizosalia ikiwmo ya Iringa , Kilolo na Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Ishengoma wa tatu kulia waliokaa akiwa na baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa na viongozi wa wilaya ya Iringa na Manispaa ya Iringa katika moja kati ya vikao vyake na wanahabari Iringa
.............................................................................................................................................
" kila waka nilikuwa nikiwasalimia kamwene ...makasi hii ni kutokana na wakazi wa mkoa huu wa Iringa kupenda zaidi kazi .....niliupenda sana mkoa wa Iringa na watu wake jinsi ambavyo walivyo na moyo wa kujituma katika kazi sitausahau mkoa wa Iringa na nitaendelea kuusemia vizuri mkoa huu wenye historia kubwa nchini" alisema Dr Ishengoma
DR Ishengoma wa pili kulia alipotembelea mabanda ya wakulima kuhamasisha kilimo
.........................................................................................................................
Kuwa akiwa mkoani Iringa amehamasisha ukuaji wa sekta ya utalii mikoa ya nyanda za juu kusini hasa mkoa wa Iringa kwa kuanzisha historia ya chifu Mkwawa na utunzaji wa kumbukumbu ya historia ya mkoa kwa kushirikianana chuo kikuu cha Iringa .
0 comments:
Post a Comment