Wednesday, 2 December 2015

BAADA ya wiki iliyopita kuwaletea marais wa Afrika waliofia madarakani. Yaani walikuwa wakiongoza nchi zao wakakumbwa na mauti. Wiki hii tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani.
View photo in message
Wageni na maafisa wa shirika la ndege la Etihad wakishiriki katika hafla ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Shirika hilo hapa nchini.
 (Washiriki)
-        Mh. Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, Balozi Wa Umoja wa falme za Kiarabu nchini Tanzania (Katikati)
-        Daniel Barranger, Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad (wa nne kulia)
-        Dr. Shaaban Mwinjaka Katibu Mkuu, Wizara Ya Uchukuzi (wa pili kulia)
-        Mh. Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania Kwa Umoja wa falme za Kiarabu (wa nne kushoto)
-        Mhandisi Thomas Haule Mkurugenzi Mamlaka ya Ndege-Tanzania (wa kwanza kushoto)
-        Ahmed Al Shehhi-Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ndege la Etihad Tanzania (wa kwanza kulia
View photo in message
Ndege iliyozinduliwa na Shirika la Ndege la Etihad ilipowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na magari ya zimamoto kwa kumwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege za shirika la ndege la Etihad lenye makao mkuu Abudhabi. Uzinduzi huo unatoa fursa sasa kwa watanzania kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.

View photo in message
Makamu wa Rais- Mauzo ya Kimataifa wa shirika la ndege la Etihad Bw. Daniel Barranger (katikati) akifurahia kikundi cha ngoma mara baada ya uzinduzi rasmi wa shirika hilo la ndege hapa nchini. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo sasa wateja mbalimbali watakua na fursa ya kusafiri moja kwa moja kutoka Dar es salaam mpaka Abudhabi kila siku.(VICTOR)

Sunday, 29 November 2015


Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL) Stanley Samtu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na (kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.


 Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (katikati) ni Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu na kulia ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL), Stanley Samtu (wa kwanza kushoto), Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (wa kwanza kulia) Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez(katikati) kwa pamoja wakiwa na mabalozi wa pombe kali ya Johnnie Walker Chiku Ally(wa pili kushoto) na Judith Mbowe(wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. “Johnnie Walker”ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.(VICTOR)

Friday, 20 February 2015

index
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia kambini siku ya jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka huu.
Kaijage ametangaza program yake ya mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.
Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume, imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.
Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.
Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.

MSAMA Promotion kwa mara nyingine tena imeandaa Tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka katika mikoa tofauti hapa nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anasema kwamba tamasha hilo mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na matamasha mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi na watakuwa wanafurahia miaka 15 tangu lianzishwe.
"Kwanza kabisa tofauti na matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje.
"Kutakuwa na waimbiaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nje ya Afrika, ambapo lengo kubwa ni kulifanya tamasha hili kuwa na utofauti," anasema.
Moja ya maboresho makuwa katika miaka 15 ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu Msama amesema kwamba litakuwa na kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
"Waimbaji wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali," anasema.
Anasema kutokana na ukumbwa na maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya maandalizi imewashirikisha watu 100, wakiwa ni wachungaji na Wainjilisti.
Anasema lengo kubwa la kuwashirikisha wachungaji na Wainjilisti ni kwa sababu watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hilo ni la kumsifu Mungu.
"Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho.
"Tutaheshimu mno maoni ya wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa lilikuwa n kiboresha tamasha letu," anasema.
Mwaka huu Tamasha la Pasaka linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.
Umaarufu wa matamasha hayo pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya nyota waliowahi kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela Chibalonza kutoka Kenya, ambaye naye aliwahi kutikisa.Baadhi ya nyimbo zake zilizotikisa na kukonga nyoyo ni Yahwe Uhimidiwe na Uliniumba Nikuabudu.
Wengine walioweka historia nchini ni pamoja na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini. Mwimbaji huyo alivunja rekodi ya waimbaji wote licha ya kuwa hafahamu lugha ya Kiswahili vilivyo, lakini aliweza kuimba nyimbo kadhaa za Kiswahili kama Mwambamwamba ili kwenda sawa na Watanzania aliokonga nyoyo zao kwa kuwapa neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.
Sipho Makhabane, Rebeka Malope nao kwa nyakati tofauti, walifanya vizuri ukiachilia mbali waimbaji wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Ambassadors of Christ (Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), 24 Elders (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).
Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Kwa upande wa Mukubwa ambate ametamba sana na wimbo wa Mfalme wa Amani amepata kutamba katika tamasha hilo na albamu mbalimbali ikiwemo ya Usikate Tamaa yenye nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Usikate Tamaa, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri.Pia ana albamu nyingine mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie.
Pia yupo msanii, Solly Mahlangu 'Obrigado' wa Afrika Kusini ambaye ingawa alitumbuiza Tamasha la Krismasi, lakini amekuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki.
Mahlangu ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.
Mbali ya kuwa maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji ambaye ana uwezo wa kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo ni Word Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.
ED_003124_564364598

Friday, 2 January 2015



Ndugu zangu....
Mpira wa miguu unaongoza duniani kuwa na mashabiki wengi zaidi.Hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika mchezo huo.
Hakika kwa sasa soka ni biashara nzuri zaidi duniani.Una shangaa nini tazama matajiri wanavyopigana vikumbo kuwania umiliki wa vilabu mbali mbali barani ulaya.
Uku wana soka kutoka Afrika magharibi wakichuana vikali kuchukua noti kutoka ulaya.Wana soka wetu wa hapa nyumbani wao wana kwenda hatua mbili wana rudi nane na kujipongeza.
Una kumbuka wakati Haruna Moshi Boban hakiwa kwenye ubora wake..?
Yeye alipata nafasi ya kusukuma kandanda barani ulaya kwenye nchi ya Sweden.Lakini kwa sasa unajua yuko wapi....Boban yuko na timu ya Friends Rangers inayoshiriki ligi daraja la kwanza.
Huu ni sawa na utani katika soka letu,ambalo limekosa mipango thabiti kutoka kwa viongozi wetu wa soka.
Lakini si hilo tu eti hata mshahara wake pale Friends Rangers analipwa na msanii wa mziki wa kizazi kipya... Diamond kiasi cha shilingi za Kitanzania 400000.Huu pia ni utani unaokera zaidi.


Mwanamfalme Andrew
Kasri ya Buckingham imepinga madai kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa alijihusisha katika tabia mbaya baada ya kubainika kwa nakala za mahakamani nchini Marekani zinazomuhusisha na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
Taarifa ya kasri hiyo imeelezea madai hayo kwamba mwanamfalme huyo alifanya tendo la ngono na msichana mdogo kama yasio kuwa ya kweli.
Mamaake mwanamfalme Andrew
Tuhuma hizo zimetolewa katika kesi inayomuhusisha rafiki moja wa zamani wa mwanamfalme Andrew, tajiri Jefferey Epstein ambaye ameshtakiwa kwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia.
Katika nakala zilizopatikana katika mahakama ya huko Florida,mwanamke mmoja anadai kwamba alilazimishwa na Epstein kufanya tendo la ngono na watu wengine akiwemo mwanamfalme huyo wakati msichana huyo alipokuwa na miaka 17,ambao ni umri mdogo wa kuweza kuruhusu tendo kama hilo nchini Marekani.


o
Rais wa Gambia yahya Jammeh aliyeepuka jaribio la mapinduzi.baadhi ya watu waliohusika na mapinduzi hao wameanza kukamatwa
Watu kadhaa wamekamatwa na kuzuiliwa, kufuatia jaribio la mapinduzi ya hapo Jumanne dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo, Yahya Jammeh.
Waliokamatwa ni pamoja na maafisa kadhaa wa kijeshi pamoja na raia.
Wanajeshi watiifu kwa rais, wanasemekana wamekuwa wakisaka nyumba za wapinzani wake.
Awali akiwa katika mji mkuu Banjul, Rais Jammeh alilaani washukiwa hao wa mapinduzi wanaosemekana kuungwa mkono na baadhi ya mataifa ya kigeni.


Mmoja ya watoto waliojeruhiwa wakati bomu liliporushwa katika nyumba moja iliokuwa ikifanya sherehe ya harusi mkoani Helmand nchini Afghanistan.Takriban watu 20 waliaga dunia
Sherehe moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya kumi na mbili.
Kisa hicho kilitokea wakati wa makabiliano makali kati ya walinda usalama wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Helmand.
Mmiliki wa jumba lilofanyiwa harusi hiyo amesema kuwa wageni walikuwa wanajikusanya nje kumkaribisha bi harusi,na kuongezea kuwa watoto wake tisa wametoweka.
Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Lashkar Gah,mji mkuu wa mkoa huo.
Shambulio hilo limetokea wakati wa siku ya mwisho kwa ujumbe wa wanajeshi wa Marekani na wale wa shirika la kujihami la NATO wanaoondoka nchini Afghanistan.


Wastara Asoma Dua Kumuenzi Sajuki
  • Wastara Asoma Dua Kumuenzi Sajuki 1
 
Mwigizaji wa filamu za Kibongo Wastara Juma leo amesoma dua  maalumu kama ishara ya kumkumbuka na kumuenzi aliyekuwa mume wake kipenzi , marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Marehemu Sajuki alifariki dunia Januari 2.2013 , ambapo leo ametimiza miaka  miwili, dua ya kumuombea ilianzia katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo marehemu Sajuki alizikwa na baadae kuhamia nyumbani kwake Tabata.
Akizungumza na GPL, Wastara alisema anajisikia faraja sana kusoma dua kwa ajili ya mtu aliyempenda lakini pia anawashukuru wadau na  wote waliojitokeza katika kufanikisha  kisomo hicho.
Aidha wasanii mbalimbali wamejitokeza akiwemo Mohamed Mwikonge ‘’Frank’ Mtitu, Nisha, Bond na wengineo ambao pia wameomba na kuwakumbusha wasanii na wadau mbalimbali kuwakumbuka na kuwaenzi wasanii pindi wanapoaga dunia.


mahakama ya kenya
Mahakama kuu nchini Kenya imesimamisha kwa muda matumizi ya baadhi ya vipengee vya sheria ya usalama yenye utata iliopitishwa na bunge na kuidhinishwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Wanasiasa wa upinzani waliwasilisha kesi mahakamani kupinga uhalali wa sheria hiyo kikatiba, huku wakisema inahujumu haki ya raia wa Kenya.
Sheria hiyo iliidhinishwa majuma mawili yaliyopita bungeni huku wabunge wa upinzani na serikali wakikabiliana kwa makonde na mateke.
Bunge la Kenya
Serikali ya Kenya inasema kuwa sheria hiyo itasaidia kukabiliana na makundi ya igaidi kama vile lile la Al-Shabab.
Lakini upinzani umeibua utata kuhusu baadhi ya vipengee, kama kile cha kuwazuilia washukiwa hadi mwaka mmoja bila ya kufunguliwa mashtaka wakisema kinahujumu uhuru wa raia.
Design by Victor Simon -