Tuesday, 30 December 2014

Mcheza mpira wa zamani Clarke Carlisle alishitakiwa kwa kosa la la kuendesha gari akiwa amelewa siku chache kabla ya kupata ajali mbaya ya kugongana roli.
Carlisle mwenye umri wa miaka 35 alipata ajali tarehe 22 na bado yuko Hospital mjini Leeds.
Polisi wa Metropolitan wamethibitisha alikua na shitaka la kuendesha akiwa kalewa mnano tarehe 20 Desemba. Na alitakiwa kufika mahakama ya Highbury Corner tarehe 20 januari .
Clarke Carlisle alivichezea vilabu vya Burnley, Queens Park Rangers, Leeds United na Northampton Town, na pia alikua mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa kulipwa.
Mke wake Gemma aliandika kwenye mtandao wa twita siku ya jumatatu"Hali yake bado ni mbaya ila tunaimani atapona tunashukuru kwa msaada wenu.
Museveni ana Janet
Kenyatta ana Margaret
Kikwete ana Salma
JayZ ana Beyonce
Odinga ana Ida
Lowassa ana Regina
Kagame ana Janette

Na wewe.... UNA___________?
Chama cha riadha Tanzania (AT) kimesema mwaka 2014 umekuwa na mafanikio katika kudhibiti utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo wake licha ya kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa kama vile michezo ya Jumuiya ya Madola iliyochezwa Glasgow, Scotland ambapo Tanzania haikupata medali.
Wakati Tanzania ikiwa haina mwanariadha aliyekamatwa na kashfa ya utumiaji madawa ya kuongeza nguvu michezoni mwaka 2014, hali imekuwa tofauti kwa majirani Kenya ambayo imeripotiwa kuwa na wanariadha 26 waliokamatwa na kuhusishwa na utumiaji licha ya kufanya vizuri kimataifa.
“ Tulitoa elimu ya kutosha kwa wanariadha wetu na siku zote tuliwaeleza kuwa mazoezi na jitihada ndio siri pekee ya ushindi na si utumiaji wa madawa”, alisema mtendaji mkuu wa riadha Tanzania, Suleiman Nyambui.
Nyambui, ambaye ni mmoja kati ya wanariadha wawili wa zamani nchini Tanzania walioweka rekodi ya kushinda medali mbili katika michuano ya Olimpiki tangu nchi ilipopata uhuru wa kisiasa mwaka 1961, alisema mwaka juzi ni mwanariadha mmoja tu aliyekamatwa katika utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.
“Tunajivunia usafi wa wanariadha wetu kwa mwaka 2014”.
“Kesi za utumiaji wa dawa nchini mwetu zinapungua kila miaka inavyokwenda”, alisema Nyambui.
Wakati Kenya ikiongoza dunia katika mbio, ripoti kutoka magazeti ya Kenya zinasema kuwa wachezaji 26 akiwamo mshindi mara mbili wa mbio za Chicago na Boston, Rita Jeptoo ambaye vipimo vilionesha ametumiwa dawa.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Valentino Mlowola
Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.
Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.
Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai. Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.
Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.


Andiko Hili la Zamaradi Limewagusa  Mastaa Wengi Hapa Bongo
     
    JIFUNZE kutokumuona mtu WA AJABU kwasababu lake limeonekana tu WAZI.. jiulize una mangapi unayoyafanya KWA SIRI KUBWA ambayo yanaweza yakashangaza ulimwengu!??? Jibu unalo... mengi!! Ila unajiona msafi sababu tu halijawa dhahiri!! Hivyo usimuone yoyote wa ajabu kwa aliyoyafanya sababu hata wewe unayafanya katika style yako.. ila una uwezo wa KUJIKAUSHA kwenye kundi la watu na kumnyooshea mtu kidole sababu yake YAMEDHIHIRIKA WAZI!!! Jiulize vipi yako yakijulikana.. kwa uyafanyayo unahisi DUNIA itakuangalia vipi!!? Usijione msafi ama mwenye haki ya kusakama mtu kwakuwa tu yako HAYAJADHIHIRIKA!!! Mfanyaji ni mfanyaji tu iwe hadharani ama gizani hivyo usije ukahukumu na kusherehekea ya mtu wakati wewe una MAZITO kuliko ya huyo yaliyodhihirika.. kuna watu wanaoheshimika SANA kwenye jamii... lakini nyuma ya pazia wanafanya vitu ambavyo hata wao wanajishangaa.. kinachowalinda ni heshima tu na kufanya kwa siri ila mwisho wa siku hakimu wetu ni mmoja tu.. aidha ufanye kwa SIRI ama DHAHIRI!! Hivyo si vizuri kujikausha kwa kumuona mwenzio wa ajabu na wewe kujiweka katika kundi la watakatifu kwakuwa tu lako halijashtukiwa.. penda kutunza siri ya mtu ili MUNGU nae akusitiri.. unapomuaibisha mtu jua hata MUNGU atakuaibisha pia.. ficha aibu za watu ili MUNGU afiche za kwako.. na usipende kufurahia na kushabikia matatizo na AIBU za wengine hali ya kuwa una za kwako nyingi zipo chimbo.. be neutral and judge no one..taratibu tutaweza..!!
    By Zamaradi Mtetema
    Mastaa wengi wameili-Repost andiko hili mitandaoni akiwemo Kajala. Hata wewe nadhani limekufaa pia.
    Undugu sio lazima uwe wa damu tu, hata kushirikiana kwenye raha na tabu nao ni undugu tena huu ndio mimi naukubali zaidi.Sote tunajua na kutambua ni jinsi gani mwingizaji Mahsein Awadh “Dr Cheni “ alivyokuwa mstari wa mbele katika kipindi chote cha sekeseke la mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael  “Lulu” ambae Dr Cheni amekuwa akimchukulia Lulu kama "mtoto" wake, hivyo hivyo Lulu amekuwa akimchukulia Dr Cheni kama "baba" na mtu wakaribu.
    Sasa kilicho nifurahisha mimi kile ambacho familia ya Lulu ilichokifanya kwenye Krismas hii, kwakuialika  familia ya Dr Cheni katika kusherekea pamoja siku kuu hiyo nyumbani kwa kina Lulu.
    Hiki ni kitu kixuri kudumisha na kuendeleza umoja wakati wote.Hongera sana Lulu na muendelee kuwa pamoja daima.
    Juu ni baadhi ya picha za wanafamilia hao siku ya tukio.
    By Mzee wa UbuyuHakika Familia ya Dr Cheni na Lulu ni Ndugu Ati!!!

    Monday, 29 December 2014

    Thea: Hatuvai Vimini Kusaka Mabwana

       
      MWIGIZAJI Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea, amesema wasanii huvaa sketi fupi ‘vimini’ wakilenga kwenda na wakati na si kujipitisha mbele ya wanaume.
      Thea aliiambia Mwanaspoti, kuwa ni kama wanatekeleza wimbo wa mwanamuziki Bwana Misosi ‘Nitoke Vipi’, lakini haimaanishi kwamba wavaaji wote ni wahuni.
      “Vimini ni ‘kiki’ tu mjini, watu wengi wanaamini ni sehemu mojawapo ya uvaaji au Nitoke Vipi kama Bwana Misosi alivyosema. Kuna watu wanaamini waigizaji tunaovaa au wanaovaa vimini wanafanya hivyo ili kutafuta biashara, ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho, kama wapo basi ni kumi kwa mmoja,” alisema Thea.
      “Vimini ni ‘kiki’ tu ya mjini. Watu wanaweza kununua filamu kwa sababu wanataka kuona paja la mtu Fulani. Hapo unakuwa umeuza filamu si mwili.”
      Mshirikishe mwe
      kikosi cha wanawake kitakachoshiriki Taifa Cup
      Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara. Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa kuanzia saa 10 jioni. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza.
      Januari 10 mwakani ndipo zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan Mwinyi), Simiyu vs Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).
      Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma vs Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi vs Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.
      Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwakani, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.
      Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.
      Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.
      Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano hayo.

      Lionel Messi
      Chama cha soka cha Hispania (LFP) kimetangaza kitampa Lionel Messi tuzo ya heshima kwa kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa la liga kwa muda wote.
      Messi amevunja Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Telmo Zarra ya kufunga Bao 251 alipofunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Sevilla.
      Rais wa chama cha soka cha Hispania Javier Tebas, amethibitisha kuwa watatoa tuzo hiyo kwa mshambuliaji huyo wa timu ya Barcelona.
      Messi atapewa Tuzo hiyo Januari 11 katika Uwanjani Nou Camp wakati Barca itakapocheza Mechi ya Atletico Madrid.
      Mpaka sasa Messi, amekwisha funga jumla ya mabao 258 katika ligi ya Hispania, huku hasimu wake wa karibu Cristiano Ronaldo akiwa nafasi ya tisa katika historia ya ufungaji bora wa muda wote.

      Jose Mourinho
      Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa kuna kampeni zinaendelea kuwashawishi waamuzi kutoa mamuzi tofauti dhidi ya timu yake.
      Mourinho amekasirishwa na mwamuzi Anthony Taylor kwa kushindwa kutoa penati katika mchezo dhidi ya Southampton ulomalizika kwa sare ya bao 1-1.
      Kiungo Cesc Fabregas alipewa kadi ya njano baada ya kuanguka katika eneo la hatari la Southampton, kwa kukwatuliwa na Matt Target na kuoneka na kama amemuhadaa mwamuzi kwa kujiangusha.
      Baada ya mchezo huo Mourinho alilamika kuwa vyombo vya habari, watangazaji mameneja wa timu zingine wote wanatoa shinikizo kwa waamuzi hivyo anadhani kuna kampeni inaoendelea dhidi ya timu yake.
      "Sijui kwa nini kuna kampeni inaendelea dhidi ya timu yangu ila sijali,kila mtu anajua ile ilikua ni penati."
      Mourinho anafahamika Zaidi kwa kwa kauli zake tata ambazo amekua akizitoa mbele ya waandishi wa habari.


      Leo ni birthday ya mkongwe wa muziki nchini Professa Jay. Hizi ni baadhi ya salamu za pongezi alizopata.
         

        Leo ni birthday ya kaka mkubwa Joseph Haule ama Professa Jay anayetimiza miaka kadhaa hapa duniani. Na hizi ndi baadhi ya salamu za pongezi alizozipata toka kwa mastaa mablimbali wa filamu na muziki nchini.

        KAJALA  -  Hbd kaka mkuu nakutakia maisha mema yenye baraka tele Professa Jay

        JACQUILNE WOLPER . Mungu Akupe Afya Njema Na Akulinde pamoja na Kuendelea Kukupa Mafanikio,Mambo Mengi Umeyafanya Kwenye Muziki Wetu. Respect Sana. Nakukubali sana kaka yangu naunajua

        FLORAH MVUNGI. Happy birthday shem akeee..Mungu akujalie maisha marefu yenye mafanikio.. Ili your daughter cute Lisa awe Nawe siku zote...all the best..! Professa Jay

        SHAMSA FORD.  happy birthday kamanda wangu..mungu akupe maisha marefu yenye baraka telee star wangu number 1


        DIAMOND PLATNUMZ . Naamini Nguzo, misingi, na heshima uliyoitengeneza kwenye tasnia yetu, ndio imepelekea hadi leo Muziki wetu kufikia hapa ulipo... Mwenyez Mungu akupe maisha maref, yenye furaha na baraka tele... Happy Birthday Legend Professa Jay

        BATULI. Mungu ana sababu yake anapoamua kukuongezea miaka mingi ya kuishi, Kaka nakutakia maisha marefu, mema na yenye baraka tele kwako, Ibada ndio zawadi kubwa ya kumpa Mungu ili nae aendelee kukupa miaka mingi zaidi "Happy Birthday Broda" Happy Birthday Professa Jay
        MWASITI . Happy bornday kaka mkubwa...live long!! Na mwenyezi akupe moyo huo huo uendelee kutupenda wadogo zako Professa Jay.
        MTAZAMO HURU.... tunapenda kukupa pongezi za dhati Professa Jay na kukutakia maisha marefu na yenye Baraka.
        Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba akiongea na wasanii....
           
        Akiwa pamoja na wasanii 
        Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
        Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
        Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

        Friday, 19 December 2014


        Wema Na Diamond Wafurahia Usiku Mmoja Jijini Kampala,Uganda
           
          Usiku wa jana tarehe 18, jiji la Kampala nchini Uganda lilipambwa na “EVENTS” mbili mkubwa kwenye upande wa buruani ambazo ni Show kubwa ya mwnamziki Jose Chameleone iliyofahamika kama  1Man Show Million na Pati ya mwanamama Zari iliyofahamika kama Zari All White Ciroc Party.
          Mwigizaji Wema Sepetu na mwanamziki Diamond Platnumuz wote walitua nchi humo na kugawana  matukio hayo kama ifuatavyo;
          Wema Sepetu ambae anadai ni amekuwa shabiki mkubwa wa masanii Jose Chameleone alitokea nchini Ghana na kutua jijini Kampala kuhudhuria show ya mwanana mziku huyo ambayo ilifanyika Serena Hotel.
          Wakati Diamond Platnumz ambae kwasasa ana “Le Project” na mwanamama Zari alihudhulia pati ya Zari kama “Special Guest”.
          Baadhi ya watu wamechukulia kitendo hiki ni kama mwanadada Wema “Amepaniki” hivi, Huku wengine wakisema kuwa Wema ana uhuru wakufanya kile anachokitaka bila ya kuhofia watu watasemaje.
          Jambo hili halijatokea kwa bahati mbaya kwani wiki kadhaa zilizopita, Diamond alipoonyesha kum-support Zari kwenye pati yake,Wema nae alibuka na kum-support Jose. Kama unavyoona hapa chini.


          19.12.2014 -  Tags:  WEMA 


          SIKU chache kabla ya kupatwa na umauti, mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ alifunguka maneno ambayo yalionesha dhahiri kama alikiona kifo chake. Kwenye mazungumzo hayo aliyozungumza na mwanahabari wetu, Aisha alisema atatoa habari nzito ambazo zitaripotiwa na magazeti matatu na kudai ni ‘sapraiz’.
          Mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’.
          Licha ya paparazi wetu kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni  sapraiz.…
          Stori: Gladness Mallya
          SIKU chache kabla ya kupatwa na umauti, mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’ alifunguka maneno ambayo yalionesha dhahiri kama alikiona kifo chake. Kwenye mazungumzo hayo aliyozungumza na mwanahabari wetu, Aisha alisema atatoa habari nzito ambazo zitaripotiwa na magazeti matatu na kudai ni ‘sapraiz’.
          Mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’.
          Licha ya paparazi wetu kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni  sapraiz.
          “Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.
          “Niko fiti nimeachana na madawa ya kulevya sasa hivi nimerudi rasmi kwenye kazi yangu ya unenguaji, nitakutafuta siku nikupe habari kubwa ambayo sijawahi kuzungumza sehemu yoyote yaani itakuwa ni nzuri na utatoa magazeti matatu,” alisema Aisha ambapo Desemba 17, mwaka huu alifariki dunia kabla ya kutimiza ahadi hiyo kwa mwandishi wetu.Aisha aliyeacha watoto wawili wa kiume na wa kike, alitarajiwa kuzikwa jana nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar.


          NAFURAHI tena kukutana na nyinyi marafiki katika uwanja wetu huu wa kujidai. Kupitia safu hii tunapata wasaa wa kushauriana masuala mbalimbali yahusuyo maisha ya uhusiano.Marafiki, leo nataka kuzungumza na nyinyi juu ya maendeleo ya teknolojia ya simu za ‘kutachi’. Simu hizi zimegeuka kuwa tatizo kubwa kutokana na wengi kuzitumia ndivyo sivyo.
          Imefika wakati simu inamteka mtu akili kiasi cha kusababisha maafa makubwa katika suala la uhusiano. Wanandoa, wachumba wamekuwa wakiingia katika migogoro kila kukicha kutokana na mmoja wao kuwa bize pindi anapokuwa na mwenzake.
          Simu hizi zimewateka akili watu wengi…
          NAFURAHI tena kukutana na nyinyi marafiki katika uwanja wetu huu wa kujidai. Kupitia safu hii tunapata wasaa wa kushauriana masuala mbalimbali yahusuyo maisha ya uhusiano.Marafiki, leo nataka kuzungumza na nyinyi juu ya maendeleo ya teknolojia ya simu za ‘kutachi’. Simu hizi zimegeuka kuwa tatizo kubwa kutokana na wengi kuzitumia ndivyo sivyo.
          Imefika wakati simu inamteka mtu akili kiasi cha kusababisha maafa makubwa katika suala la uhusiano. Wanandoa, wachumba wamekuwa wakiingia katika migogoro kila kukicha kutokana na mmoja wao kuwa bize pindi anapokuwa na mwenzake.
          Simu hizi zimewateka akili watu wengi kiasi kwamba kila wakati mtu anataka kubofya au kupangusa kama vijana wanavyosema. Atataka kupangusa akiwa kazini, akiwa katika usafiri wa umma au wa binafsi na hata akifika nyumbani na kukutana na mpenzi wake ataendelea kufanya hivyo.
          Hata kama ametoka ‘out’ na mpenzi wake, bado mtu wa aina hiyo utamuona anaongea maneno machache na mwenzake huku muda mwingi akiuutumia kuperuzi mitandao mbalimbali tena mbaya zaidi mingi ni ya umbeaumbea tu!
          Ukiachana na suala la kuperuzi mitandao, tathmini isiyo rasmi inaonesha miongoni mwa vitu vinavyowapotezea muda mwingi watu katika simu hizo ni matumizi ya magrupu ya mitandao mbalimbali ambayo wanayaanzisha kwa kundi la watu fulani.
          Eti utasikia hili grupu la wafanyakazi wenzangu, hili ni la wanandugu na lingine ni la kufundisha mambo fulanifulani wanayoyajua wenyewe. Hayana maana yoyote!Wataanzisha kundi ambalo linamlazimu kujibu au kuchangia mjadala fulani ambao pengine umeanzishwa na kumhusisha yeye hivyo hawezi kukubali kukaa kimya pindi wenzake wanapochangia.
          Asilimia kubwa ya mijadala ambayo inaonekana kupendwa zaidi na watu inaonekana si yenye tija, wanapenda vitu vya umbeaumbea kujua fulani anatoka na nani au fulani kammwaga fulani.
          Vitu hivyo vinawafanya wanawehuka kabisa, maana mtu hujikuta hata akikosea maneno pindi anapoongea na mpenzi wake na kutaja neno ambalo alikuwa akiliandika katika grupu alilokuwa akichangia kupitia simu yake hiyo ya kisasa.
          Kwa jinsi alivyonogewa na umbea, anasahau kabisa kwamba mumewe anapaswa kupelekewa maji bafuni au kuandaliwa chakula, achilia mbali vile vikorombwezo vya kimahaba ambavyo wapendanao wanapaswa kupeana pindi wanapokuwa pamoja hususan nyumbani au chumbani.
          Ili asipitwe na mjadala kwenye grupu fulani, yuko radhi amuite hausigeli na kumtuma amfanyie kila kitu ambacho kilipaswa kufanywa na yeye.Achilia mbali masuala ya mapenzi, kuna wakati mwenzake atataka kukaa na kujadili mambo ya kifamilia, suala hilo pia linaweza kushindikana eti tu kwa sababu mwenzake yuko bize na simu.
          Tatizo hapa linakuwa ni aina ya mtu ambaye utakuwa naye. Kuna mtu anaweza kukutolea uvivu na kukwambia kwamba unamkwaza kutokana na kitendo chako cha kutomjali lakini kuna mwingine hawezi, atakaa nalo moyoni na kufanya maamuzi yake anayoyajua mwenyewe.
          Itaendelea wiki ijayo.


          Stori: Imelda Mtema

          STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
          Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
          Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
          “Nilijaribu kuweka…Stori: Imelda Mtema

          STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
          Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
          Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
          “Nilijaribu kuweka…Stori: Imelda Mtema

          STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
          Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
          Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
          “Nilijaribu kuweka…VStori: Imelda Mtema

          STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
          Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
          Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
          “Nilijaribu kuweka…Stori: Imelda Mtema

          STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
          Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
          Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.


          “Nilijaribu kuweka mawigi pembeni na kujisukia tano kichwa changu kwa kweli naonekana katoto kabisa hapo ndipo nilipogundua kuwa mawigi kwa kipindi kingine siyo kabisa yanatuzeesha tu,” alisema Lulu.
          Design by Victor Simon -