Friday, 19 December 2014


JOHARI: Sina Matatizo ya Kizazi, Nitazaa Nikiolewa
     

    <div data-blogger-escaped-trbidi="on" dir="ltr" left;"="">

    Mwigizaji nguli wa filamu hapa nchini, Blandina Chagula  "Johari" amekanusha tetesi na uvumi kuwa anamatatizo ya kizazi na hivyo hawezi kushika ujauzito,kwa kueleza kuwa kizazi chake kinafanya kazi na anachosubiri ni kumpata mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa ndipo atakaporuhusu kuzalishwa.
    Akizungumza na mwandishi wa GPL, Johari alisema kuwa endapo akitokea tayari yupo ndani ya ndoa anaweza kufanya hivyo lakini kwa maneno ya watu kamwe watasubiri kwani anaamini kizazi chake kipo imara na wakati wowote akiamua kushika mimba kitafanya kazi.
    “Kizazi changu kinafanya kazi na mipango hiyo ya kushika mimba mimi siwezi kukubali nipate mtoto kabla ya kuolewa, suala la kufanya jambo kwa lengo la kuwafurahisha watu mimi siwezi kufanya hivyo,” alisema Johari.
     Pichani ni Johari akiwa na mtoto wa Irene Uwoya, Krish

    0 comments:

    Post a Comment

    Design by Victor Simon -