
Chama cha riadha Tanzania (AT) kimesema mwaka 2014 umekuwa na mafanikio katika kudhibiti utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo wake licha ya kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa kama vile michezo ya Jumuiya ya Madola iliyochezwa Glasgow, Scotland ambapo Tanzania haikupata medali.
Wakati Tanzania ikiwa haina mwanariadha aliyekamatwa na kashfa ya utumiaji madawa ya kuongeza nguvu michezoni mwaka 2014, hali imekuwa tofauti kwa majirani Kenya ambayo imeripotiwa kuwa na wanariadha 26 waliokamatwa na kuhusishwa na utumiaji licha ya kufanya vizuri kimataifa.
“ Tulitoa elimu ya kutosha kwa wanariadha wetu na siku zote tuliwaeleza kuwa mazoezi na jitihada ndio siri pekee ya ushindi na si utumiaji wa madawa”, alisema mtendaji mkuu wa riadha Tanzania, Suleiman Nyambui.
Nyambui, ambaye ni mmoja kati ya wanariadha wawili wa zamani nchini Tanzania walioweka rekodi ya kushinda medali mbili katika michuano ya Olimpiki tangu nchi ilipopata uhuru wa kisiasa mwaka 1961, alisema mwaka juzi ni mwanariadha mmoja tu aliyekamatwa katika utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu.
“Tunajivunia usafi wa wanariadha wetu kwa mwaka 2014”.
“Kesi za utumiaji wa dawa nchini mwetu zinapungua kila miaka inavyokwenda”, alisema Nyambui.
Wakati Kenya ikiongoza dunia katika mbio, ripoti kutoka magazeti ya Kenya zinasema kuwa wachezaji 26 akiwamo mshindi mara mbili wa mbio za Chicago na Boston, Rita Jeptoo ambaye vipimo vilionesha ametumiwa dawa.
0 comments:
Post a Comment