Muigizaji na muongozaji wa filamu Vicent Kigosi “Ray” akiongea kwenye kipindi cha Television cha Boys Boys kinachorushwa na kituo cha TV1. Alionekana kupinga swala watu wenye pesa zao lakini bado wanasumbua watu kwa michango ya harusi hivyo akashauri ni bora mtu kabla ya kuoa ajipange na sio kusumbua watuna kadi za michango.
“Sio mtu unawapa watu mizigo isiyo ya kwao,” alisema. “Kama una uwezo fanya mwenyewe, kwa sababu katika maisha tunaambiwa kuna vitu vitatu, kuzaliwa, harusi na mwisho kifo! Sasa kama una uwezo, fanya kitu kikubwa zaidi katika maisha yako, lakini sio michango nikikutana na meseji ya mchango, hata kupokea simu inakuwa shida,”
Pichani ni Ray akiwa na mpenzi wake Chuchu.
0 comments:
Post a Comment