Undugu sio lazima uwe wa damu tu, hata kushirikiana kwenye raha na tabu nao ni undugu tena huu ndio mimi naukubali zaidi.Sote tunajua na kutambua ni jinsi gani mwingizaji Mahsein Awadh “Dr Cheni “ alivyokuwa mstari wa mbele katika kipindi chote cha sekeseke la mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael “Lulu” ambae Dr Cheni amekuwa akimchukulia Lulu kama "mtoto" wake, hivyo hivyo Lulu amekuwa akimchukulia Dr Cheni kama "baba" na mtu wakaribu.
Sasa kilicho nifurahisha mimi kile ambacho familia ya Lulu ilichokifanya kwenye Krismas hii, kwakuialika familia ya Dr Cheni katika kusherekea pamoja siku kuu hiyo nyumbani kwa kina Lulu.
Hiki ni kitu kixuri kudumisha na kuendeleza umoja wakati wote.Hongera sana Lulu na muendelee kuwa pamoja daima.
Juu ni baadhi ya picha za wanafamilia hao siku ya tukio.
By Mzee wa Ubuyu
0 comments:
Post a Comment