Tuesday, 16 December 2014

Yanga Wamalizana Na Maximo
Kocha mkuu wa klabu ya Dar es salaam Young Africans Marcio Maximo amekubaliana na viongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake na huenda akaondoka nchini ndani ya siku tatu zijazo.
Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini baada ya kufanya mazungumzo kwa kina juu ya kuvunjwa kwa mkataba wake na hatimae muafaka umepatikana.
Maximo anaondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, wakati Pluijm anawasili usiku huu na kesho atasaini Mkataba na kuanza kazi. Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni. Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.

0 comments:

Post a Comment

Design by Victor Simon -