
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mshambuliaji Dan Sserunkuma anatarajiwa kutua nchini kesho kumalizana na Simba ili achukue nafasi ya Mkenya Paul Kiongera ambaye ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC msimu huu kutokana na majeraha.
Uongozi wa Gor Mahia ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) umethibitisha kumpoteza mfumania nyavu huyo hatari — Sserunkuma, ukieleza kuwa umezidiwa kete na wanamsimbazi.
Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kutolewa ripoti zisizo rasmi za Sserunkuma kutua Simba, leo Gor imetoa taarifa rasmi ikiweka wazi kwamba mkataba wake na klabu hiyo uko karibu kumalizika na amekataa kusaini mkataba mpya.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Gor Mahia Chris Omondi, mshambuliaji huyo amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea na mabingwa hao wa KPL kwa vile amepata ofa nono kutoka Simba, ambayo Gor hawakuwa na jinsi ya kumpa zaidi ya kumwachia aende Tanzania
0 comments:
Post a Comment