Saturday, 6 December 2014


23B70FA100000578-2862210-He_has_covered_more_than_100_miles_this_season_with_Chelsea_unbe-a-1_1417786977347
Mchezo wa soka kwa miaka ya karibuni umekuwa ukibadilika kwa kasi huku ushindani wa mchezaji kwa mchezaji na timu dhidi ya timu nyingine ukizidi kuongezeka .
Hali hii inamaanisha kuwa wachezaji ambao kimsingi wanalipwa fedha nyingi sana wanalazimika kujituma mara mbili au zaidi ili kuweza kutimiza malengo ya timu zao.
Katika kudhihirisha hili wachezaji walio bora hupimwa kwa kutumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu na kinachowahukumu katika ubora au ubovu wao ni takwimu ambazo hufichua kile ambacho mchezaji anakifanya akiwa kwenye uwanja wa mazoezi na hata wakati wa mechi .
Takwimu kwenye ligi ya England zinaonyesha kuwa kiungo Mhispania wa Chelsea Cesc fabregas ndio mchezaji aliyekimbia umbali mrefu kuliko wote katika michezo yote ambayo Chelsea imecheza msimu huu .
Takwimu zinaonyesha kuwa Cesc hadi sasa amekimbia zaidi kilomita 100 katika michezo yote aliyoichezea Chelsea kwenye ligi ya England msimu huu hali inayoonyesha kiwango kikubwa cha kujituma anapokuwa uwanjani .
Fabregas alifiisha kiwango hicho katika mchezo ambao Chelsea ilishinda 3-0 dhidi ya Tottenham jumatano iliyopita na hii ina maana kuwa katika mchezo ambao Chelsea imefungwa na Newcastle aliongeza na kufikisha zaidi ya kilometa 100 .
Wachezaji wengine ambao wametimiza kilomita kia moja ya eneo walilokimbia katika katika michezo ya timu zao msimu huu ni kiungo mwingine wa Chelsea Nemanja Matic na beki wa Hull city Jake Livermore.

Kiungo mwingine wa Chelsea Nemanja Matic anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji waliokimbia umbali mrefu kwenye ligi ya England msimu huu.
Kiungo mwingine wa Chelsea Nemanja Matic anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji waliokimbia umbali mrefu kwenye ligi ya England msimu huu.
Kiungo wa Hull Jake Livemore anakamilisha orodha hii ya wachezaji pekee waliokimbia umbali wa zaidi ya kilimoita 100.
Kiungo wa Hull Jake Livemore anakamilisha orodha hii ya wachezaji pekee waliokimbia umbali wa zaidi ya kilimoita 100.

0 comments:

Post a Comment

Design by Victor Simon -