Wednesday, 3 December 2014

Ndugu Zangu Leo nimepata mualiko kwenye kipindi cha Ramani ya ulimwengu kinachorushwa kila siku kuanzia saa 17:00-17:30 Ebony Fm Radio ya Mkoani Iringa kwa kuchambua mambo yahusuyo Siku ya walemavu Dunia ambayo hii leo yameadhimishwa Kitaifa hapa Tanzania katika uwanja wa Kichanganyi Mkoani Iringa huku kauli mbiu yake ikiwa ni "MAENDELEO ENDELEVU AHADI YA TEKNOLOJIA"

Yapo mengi niliyozungumza lakini zaidi ni kuhusu waandishi wa habari kupatiwa mafunzo kwa ajili ya kuripoti mambo yahusuyo unyanyasaji wa watu wenye ulemavu Tanzania
lakini pia Chama Cha Watu wenye ulemavu Tanzania (CHAWATA) wameomba sheria ibadilishwe ili kiwe chama huru tofauti na hivi sasa kilivyo chini ya Ofisi ya ustawi wa jamii.
Maadhimisho haya mwaka 2012 yalifanyika Musoma-Mara ambapo kauli mbiu yake ilikuwa ni "ONDOSHA VIKWAZO ILI KUJENGA JAMII NA UFANISI KWA WOTE"
Aidha mwaka wa jana yalifanyika pia katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prf Jakaya Mrisho Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.
Maadhimisho haya yamekuwa yakifanyika kila mwaka tarehe 3/12 kwa muktadha wa ufanisi na kutambua umuhimu wa watu wenye ulemavu kuwa binadamu wote ni sawa.
Pichani nipo na Mtangazaji wa Ebony Fm Festus Pangani wa Ramani ya Ulimwengu nikiwa naye Ofisi za Ebony Fm lakini pia picha ya baadhi ya walemavu waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo.
Naam, Uchambuzi wa habari unahitaji kuchimba
Mathias Canal
0756413465
Iringa

0 comments:

Post a Comment

Design by Victor Simon -