Wednesday, 10 December 2014

ZAMARADI: Nategemea kazi bora kutoka kwa Wema na Van Vicker
Mtangazaji na wa kipindi cha television cha maswala ya filamu,TAKEONE, kinachorusha na kituo cha CloudsTV, Zamaradi Mtetema baada ya hivi majuzi kutoa maoni yake juu ya tasnia hii ya filamu hapa nchini[SOMA HAPA], ambayo yaliozua mjadala mrefu miongoni mwawadau wa tasnia hii.
Leo ameibuka na kuonekana kuwa mwenye shauku kubwa na matumaini makubwa ya kazi anayoifanya muigizaji Wema Sepetu huko nchini Ghana. Zamaradi kupitia ukurasa wake aliandika;
Baada ya kuandika hivyo mashabiki wengi walionyesha kukubaliana naye na wengi kudaikuwa hii project itoke mapema zaidi kwani watu wamem-MISS sana Wema.
Muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu hivi sasa yupo nchini Ghana kwaajili ya utengenezaji wa kazi mpya akifanya na muigizaji na muongozaji wa filamu wa nchini humo, Joseph Van Vicker .
Kazi hiyo inafanyika chini ya  ENDLESS FAME, kampuni ya Wema mwenye. Tuendelee kuisubiri jamani.

0 comments:

Post a Comment

Design by Victor Simon -